
Rais Samia Suluhu Hassan tarehe 01 Februari 2022 amemteua mwanahabari maarufu Zuhura Yunus kuwa Mkurugenzi mpya wa Mawasiliano ya Rais. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais aliyemaliza muda wake, Jaffar Haniu, uteuzi huo unaanza mara moja. Kabla ya kuteuliwa katika ofisi ya umma, Yunus alifanya kazi kama Mtayarishaji na Mtangazaji katika Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC). Anakuwa mwanamke wa kwanza kushika nafasi hiyo. Bw Haniu alihudumu katika nafasi hiyo kama Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais tangu Juni 9, 2021 alipoteuliwa na Rais Samia.