habari kmli

: Walinda amani wanane wa Umoja wa Mataifa katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya #Congo (MUNUSCO) wamefariki dunia wakati helikopta yao ilipoanguka karibu na mpaka na #Rwanda siku ya Jumanne.

Jeshi la Congo lilishutumu wapiganaji wa vuguvugu la Machi 23 kuiangusha helikopta hiyo, hata hivyo waasi wamekana kuhusika.

MONUSCO ilisema kuwa helikopta ya Pakistan yenye namba 810 ilikuwa katika safari ya upelelezi juu ya Tshanzu, katika Mkoa wa Kivu Kaskazini, karibu na mpaka wa Rwanda na #Uganda.

Ilianguka Jumanne katika eneo linalodhibitiwa na waasi, wanaojulikana kama M23, kulingana na taarifa ya msemaji wa jeshi la Congo Jenerali Sylvain Ekenge.

Mbali na wafanyakazi sita wa Pakistani, helikopta hiyo ilimbeba Luteni Kanali Alexey Mizyura wa #Urusi na Luteni Kanali Dejan Stanojevic wa #Serbia, wote wakihudumu na MONUSCO. Jeshi la #Pakistan lilisema wote wanane walifariki katika ajali hiyo, lakini hawakutaja sababu.

#somethingforeveryone
#kigomafahariyetu
#radiojoydigital

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *