
Serikali ya Marekani Imeahidi Kuendelea Kutoa Ushirikiano Kwa Serikali Ya Tanzania Katika Kuendelea Kufadhili Miradi Mbalimabli Ya Kimaendeleo Baina Ya Serikali Hizo Mbili.
Hayo Yamesemwa na Balozi Wa Marekani Nchini Tanzania Balozi Donald Wright Wakati Wa Mahojiano Katika Kipindi Maalum na Radio Joy na kueleza kuwa Wamekuwa Wakifanya Kazi Za Kusaidia Jamii Kupitia Mashirika Mbalimbali Zikiwemo Mazingira, Afya, Wanawake na Watoto.
Aidha Ameupongeza Uongozi wa Rais Wa Jamuhuri Wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hasan kwa Hatua Anazo zichukua Dhidi ya Kupambana na Ugonjwa wa Uviko 19.
Aidha Amesema Kwa Sasa Serikali ya Marekani Imejikita Zaidi Katika Mambo Matatu Ambayo ni Kutokomeza Ugonjwa Wa Ukimwi, Utunzaji Wa Mazingira Na huduma bora Kwa Wakimbizi Waliopo Mkoani Kigoma.