
Uongozi wa klabu ya Ruvu Shooting umeweka wazi Kocha Mkuu mpya Mbwana Makataa ambaye atakuwa ndani ya kikosi hicho tangu sasa.
Amepewa mkataba wa mwaka mmoja akibeba mikoba iliyoachwa wazi na Charles Boniface Mkwasa ambaye alijiuzulu nafasi yake hapo jana, Desemba 5,2022 kutokana na mwenendo mbaya wa matokeo katika mzungumko wa kwanza wa ligi kuu ambao umemalizika hivi karibuni.
Mchezo wake wa mwisho kukaa kwenye benchi la ufundi timu yake ilipoteza kwa kufungwa mabao 2-1 dhidi ya Dodoma Jiji, timu ambayo Makata aliwahi kuifundisha.
Timu yake ya mwisho kuinoa Makata ilikuwa ni Mbeya Kwanza iliyoshuka daraja ambapo aliwahi kukutana na adhabu ya kufungiwa miaka mitano.
Adhabu hiyo ilipunguzwa kutokana na Makata kuomba msamaha kwa makosa ambayo aliyafanya jambo lililopelekea akapunguziwa adhabu hiyo.