
Pichani ni Georgina Rodriguez na Ivana Rodriguez, Gio ni Mpenzi wa Cristiano Ronaldo na huyo Ivana (pichani kulia) ni Shemeji yake Ronaldo, Wanawake hawa taifa lao ni Argentina ila makuzi yao ni Hispania kwenye mji unaitwa Jaca.
Tangu 2018 World Cup wao hawajawahi kushabikia taifa tofauti na Ureno ambalo kimsingi ni la Mume wao, juzi kwenye post ya Ivana aliulizwa swali kuwa wakikutana Ureno na Argentina yupo timu gani? Akajibu yupo Ureno, akaulizwa Ureno na Hispania? Akajibu yeye ni Ureno.
Naam! Dada mtu hataki utani linapokuja suala la Baby wao, linapokuja suala la CR7 wao ni Wareno na si vinginevyo😀