taleban

Watu 12, wakiwemo wanawake watatu, wamechapwa viboko mbele ya maelfu ya watazamaji kwenye uwanja wa mpira nchini Afghanistan

Kundi hilo lilikuwa na hatia ya “uhalifu wa kimaadili” ikiwa ni pamoja na uzinzi, wizi na ngono ya mashoga, afisa wa Taliban alisema.

Hii inadhaniwa kuwa ni mara ya pili ndani ya mwezi mmoja kundi hilo la Kiislamu kufanya mashambulizi ya viboko hadharani.

Omar Mansoor Mujahid, msemaji wa Taliban wa eneo la Logar mashariki mwa Afghanistan, ambapo shambulio hilo lilitokea, alisema kuwa wanawake wote watatu waliachiliwa baada ya kuadhibiwa. Baadhi ya wanaume hao walifungwa jela, alisema, lakini haijulikani ni wangapi.

Wanaume na wanawake hao walichapwa viboko kati ya 21 na 39 kila mmoja. Idadi ya juu ambayo mtu anaweza kupokea ni 39, afisa mwingine wa Taliban alisema. Watu 19 pia waliadhibiwa wiki iliyopita katika kuchapwa viboko sawa na hivyo katika jimbo la Takhar kaskazini mwa Afghanistan, ripoti zinasema.

Kuchapwa viboko katika jimbo la Logar kunakuja wiki moja baada ya kiongozi mkuu wa kundi la Taliban, Hibatullah Akhundzada, kuwaamuru majaji kutekeleza adhabu kwa baadhi ya makosa ya jinai kuambatana na usomaji mkali wa kundi hilo wa sheria za Kiislamu.

Tafsiri hii ya sheria ya Kiislamu inajumuisha kunyongwa hadharani, kukatwa viungo hadharani na kupigwa mawe – ingawa uhalifu kamili na adhabu zinazolingana hazijafafanuliwa rasmi na Taliban.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *