Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu imetoa mikopo yenye thamani ya shilingi 608,965,100 kwa vikundi 53 vya wajasiriamali kupitia asilimia 10 ya mapato ya ndani ya halmashauri, ikiwa ni sehemu ya kuwawezesha wanawake, vijana na watu wenye ulemavu kujikwamua kiuchumi. Akizungumza katika hafla ya utoaji wa mikopo ya robo ya tatu na ya nne ya mwaka wa fedha 2025/2026, kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa…