
Tanzania na Uganda zimeanza kutekeleza ujenzi wa bomba la mafuta ghafi lenye urefu wa zaidi ya kilomita 1,400 unaotarajiwa kukamilika ifikapo mwaka 2025. Mradi huo utagharimu zaidi ya dola za Marekani bilioni 5 na unatarajiwa kuzalisha zaidi ya mapipa bilioni moja kwa kipindi cha miaka 25 ijayo.