Frenkie-de-Jong-Manchester-United-scaled

Mchezaji anayelengwa na Manchester United Frenkie de Jong hataki kuondoka Barcelona – lakini iwapo atahama, kiungo huyo wa kati wa Uholanzi, 25, angependelea kujiunga na Bayern Munich au Chelsea kuliko The Red Devils. (Sport – in Spanish)

Jules Kounde anatazamiwa kufanyiwa uchunguzi wa kimatibabu wa Chelsea ndani ya saa 48 zijazo baada ya The Blues kuafikiana na Sevilla kwa ada ya pauni milioni 55 kwa ajili ya kumnunua mlinzi huyo wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 23. (Sun)

The Blues pia wamemfanya mlinzi wa RB Leipzig mwenye umri wa miaka 20 kutoka Croatia Josko Gvardiol kuwa mlengwa wao mkuu kuchukua nafasi ya beki wa pembeni wa Uhispania Cesar Azpilicueta, 32, ambaye anatarajiwa kujiunga na Barcelona.  (Sun)

Nottingham Forest inafikiria kumnunua mshambuliaji wa Watford raia wa Nigeria Emmanuel Dennis, 24, ambaye thamani yake inakadiriwa kuwa £25m.  (Mail)

th

CHANZO CHA PICHA, GETTY IMAGES

Leicester wamekataa dau la pauni milioni 15 kutoka kwa Monaco kwa ajili ya kumnunua Boubakary Soumare kwani wanataka kurejesha zaidi ya pauni milioni 23 walizotumia kumnunua kiungo huyo wa kati Mfaransa mwenye umri wa miaka 23 msimu uliopita.  (Mail)

Manchester United bado inamtaka winga wa Ajax Mbrazil Antony, 22, licha ya kwamba dau la pauni milioni 51 lilikataliwa. (Talksport)

The Foxes wanapaswa kuuza wachezaji kabla ya kununua, kwa hivyo wanaweza kufikiria ofa kwa kiungo wa kati wa Uingereza James Maddison, 25, fowadi wa Nigeria Kelechi Iheanacho, 25, na beki wa pembeni wa Ubelgiji Timothy Castagne, 26.  (Telegraph – subscription required)

TH

CHANZO CHA PICHA, GETTY IMAGES

Barcelona wamemtambua Mchezaji wa Tottenham Sergio Reguilon, 25, kama beki mbadala wa kushoto anayelengwa kama hawatakubali makubaliano na Chelsea kumnunua Mhispania mwenzake Marcos Alonso, 31. (Mundo Deportivo – in Spanish)

Brighton wanafikiria kumnunua kwa mkopo beki wa kushoto wa Arsenal Mreno mwenye umri wa miaka 22 Nuno Tavares huku wakitafuta mbadala wa mlinzi anayelengwa na Manchester City na Mhispania Marc Cucurella, 23. . (O Jogo – in Portuguese) 

Newcastle wametoa ofa ya takriban £18m kumnunua winga wa Leeds United Muingereza Jack Harrison, 25.  (Football Insider)

Nottingham Forest imempa mchezaji huru Jesse Lingard kandarasi yenye thamani ya pauni 200,000 kwa wiki huku wakipania kuwashinda West Ham katika kuinasa saini ya mshambuliaji huyo wa Uingereza mwenye umri wa miaka 29. . (Mail)

West Ham na Crystal Palace wamewasiliana na Burnley kumnunua kiungo wao Mwingereza mwenye umri wa miaka 22 Dwight McNeil. (Sky Sports)

West Ham, Everton, Napoli na Sevilla wanafikiria kumnunua winga wa Ubelgiji Adnan Januzaj, 27, ambaye ni mchezaji huru baada ya kuondoka Real Sociedad mwishoni mwa msimu uliopita.  (AS – in Spanish)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *