

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES
Manchester United wako tayari kupambana na Chelsea kwa ajili ya kumchukua mshambuliaji Mgabon kutoka Barcelona mwenye umri wa miaka 33- Pierre-Emerick Aubameyang. (Sun)
Manchester United wanaangalia uwezekano wa uhamisho wa mchezaji wa Leicester Jamie Vardy, 35, lakini mbweha wanasemekana kusita sita kumruhusu mshambuliaji huyo Muingereza kuondoka . (Athletic via Daily Star)

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES
Meneja wa Manchester United Erik ten Hag amejiandaa kumruhusu mshambuliaji Mreno Cristiano Ronaldo, 37, kuondoka katika klabu hiyo . (Times – subscription required)
Chelsea wamejipanga kuboresha ofa yao ya pauni milioni 45 kwa ajili ya winga wa Everton Muingereza Anthony Gordon, baada ya kuona kuwa da u la kwanza la pauni milioni 45 kwa ajili ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21 limekataliwa. (Times – subscription required)

CHANZO CHA PICHA,REX FEATURES
Crystal Palace wanajiandaa kulipa pauni milioni 12 kwa ajili ya mshambuliji Mghana Antoine Semenyo, huku kukiwa na nia na mchezaji huyo kutoka Bournemouth na Everton. (Mail)
Kiungo wa kati wa Sporting na mchezaji wa kimataifa wa Ureno Matheus Nunes amejiunga na Wolves kwa rekodi ya malipo ya juu ya euro milioni 45 (£38m). Liverpool na West Ham zimekuwa zikihusishwa na mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23. (Record – in Portuguese)

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES
Chelsea pia wanakaribia kushinda kinyang’anyiro cha kumchukua kiungo wa kati wa Inter Milan mwenye umri wa miaka 19-Muitalia Cesare Casadei. (Guardian)
Ofa ya Newcastle ya £20m kwa ajili ya mshambuliaji wa Watford Joao Pedro, 20, imekataliwa, huku the Hornets ikisisitiza kuwa mshambuliaji huyo Mbrazili hauzwi. (Sky Sports)

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES
West Ham wamewasiliana na Chelsea kwa ajili ya kusaini mkataba na kiungo wao wa nyuma- kushoto mwenye umri wa miaka 28 Muitalia Emerson Palmieri. (Fabrizio Romano)
West Ham pia wana nia na mlinzi wa Paris St-Germain Mjerumani Thilo Kehrer, 25, huku wakijaribu kupambana kuimarisha kikosi chao cha ulinzi. (Sun)

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES
West Ham pia wana nia na mlinzi wa Paris St-Germain Mjerumani Thilo Kehrer, 25, huku wakijaribu kupambana kuimarisha kikosi chao cha ulinzi. (Sun)
Ofa ya Manchester United ya kumnunua kiungo wa safu ya ulinzi Mholanzi Frenkie de Jong, 25, kutoka Barcelonakwa sasa imepitwa na wakati. (Kick-off of De Telegraaf via Mail)
Lakini United wako tayari kusiani mkataba na mshambuliaji Mbrazili Matheus Cunha, 23, kutoka Atletico Madrid kwa pauni £42.5m. (Express)

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES
West Ham, Marseille na Monaco wana nia ya kumchukua mlinzi wa Manchester United Eric Bailly, huku Old Trafford wakiwa makini kumuachilia kijana huyo mwenye umri wa miaka 28 raia wa Ivory Coast. (Athletic via Sun)
Mchezaji wa Chelsea Marcos Alonso ameafikiana na Barcelona kisheria na klabu hiyo ya upande wa Ligi ya La Liga side wako tayari kulipa pauni milioni 65 kwa ajili ya mlinzi huyo Muhispania mwenye umri wa miaka 31. (Bild via Sun)