

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES
Paris St-Germain wako kwenye mazungumzo na wawakilishi wa Marcus Rashford kuhusu uwezekano wa kumsajili mshambuliaji huyo wa Uingereza, 24, kutoka Manchester United. (L’Equipe – kwa Kifaransa)
United pia wana mkutano ulioratibiwa na mamake Adrien Rabiot na wakala wake baada ya kukubaliana ada na Juventus kumnunua kiungo wa kati wa Ufaransa, 27. (Fabrizio Romano).
Manchester City wana nia ya kumsajili beki wa kushoto wa Atletico Madrid wa Brazil Renan Lodi, 24. (Telegraph – usajili unahitajika)
Beki wa kushoto wa Arsenal Kieran Tierney, 25, pia ni miongoni mwa majina kwenye orodha ya wanaowania Manchester City. (90 Minutes)
Mshambulizi wa zamani wa Arsenal na Gabon Pierre-Emerick Aubameyang, 33, angependelea kusalia Barcelona kuliko kurejea katika Ligi ya Premia akiwa na Chelsea. (Sport, via Metro)
Nottingham Forest wamewasilisha ombi la kwanza kwa mshambuliaji wa Watford na Nigeria Emmanuel Dennis, 24. (The Athletic).

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES
Atalanta itachuana na Forest katika kumsajili winga wa Italia Emerson Palmieri, 28, kutoka Chelsea. (Standard)
Everton wanatarajia kukamilisha dili la kumsajili mshambuliaji wa Guinea Serhou Guirassy, 26, kutoka Rennes kabla ya mwisho wa juma. (L’Equipe – kwa Kifaransa)
Che Adams wa Southampton ana nia ya kutaka kuhamia Everton, lakini kuna ushindani kutoka kwa Leeds United, Wolves na Forest kwa mshambuliaji huyo wa Scotland, 26. (Mail).

CHANZO CHA PICHA,SNS
Aliyekuwa mkufunzi wa muda wa Manchester United Ralf Rangnick amependekeza kwamba mshambuliaji wa Stuttgart na Austria Sasa Kalajdzic, 25, anapaswa kukataa kuhamia Old Trafford. (Star)
Juventus wanakaribia kukamilisha dili la kumnunua mshambuiaji wa Barcelona na Uholanzi Memphis Depay, 28. (90min).
Marseille wamefanya mawasiliano na Manchester United kuhusu mkataba wa mkopo wa beki wa Ivory Coast Eric Bailly, 28. (L’Equipe – in French)

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES
Winga wa Bayer Leverkusen Mhispania Iker Bravo, 17, atajiunga na Real Madrid kwa mkopo wa msimu mzima. (Bild – kwa Kijerumani)
Mshambuliaji wa zamani wa Chelsea na Uhispania Diego Costa, 33, anarejea Rayo Vallecano baada ya kutokuwa na klabu tangu kandarasi yake ya Atletico Mineiro ilipomalizika mwezi Januari. (Marca)