Rabiot

Kiungo wa kati wa Ufaransa Adrien Rabiot

Manchester United wamefikia makubaliano na Juventus juu ya ununuzi wa kiungo wa kati wa Ufaransa Adrien Rabiot, 27, kwa dau la awali la £15m. (Guardian)

United pia wamemuulizia kiungo wa kati wa Real Betis na Argentina Guido Rodriguez, 28. (AS – kwa Kihispania)

Kiungo wa kati wa Lazio na Serbia Sergej Milinkovic-Savic, 27, pia bado yuko kwemye orodha ya wachezaji wamaonyatiwa na United. (Telegraph – usajili inahitajika)

Mshambuliaji wa Slovenia Benjamin Sesko, 19,

Mshambuliaji wa Slovenia Benjamin Sesko, 19.

Mchezaji mwingine anayelengwa na United, ni mshambuliaji wa Slovenia Benjamin Sesko, 19, mbaye anakaribia kukubali mkataba wa kujiunga na RB Leipzig kutoka Red Bull Salzburg mwaka 2023. (90min)

Chealse wanajiandaa kutoa ada ya juu zaidi duniani katika jitihada za kumsajili beki wa Ufaransa Wesley Fofana, 21, kutoka Leicester City. (Football London)

Mshambuliaji wa Chelsea Mjrumani Timo Werner, 26, atafanyiwa uchunguzi wa kimatibabu leo Jumanne kabla ya kurejea RB Leipzig. (Mail)ge

Timo Werner Mshambuliaji wa Chelsea Mjrumani Timo Werner kufanyiwa uchunguzi wa kimatibabu.

The Blues kwa sasa wanapungukiwa na £10m kuliko Leicester kumnunua Fofana. (Independent)

Roma wamekataa ombi la Tottenham kumnunua winga wa Italia Nicolo Zaniolo, 23, kwa mkopo wenye kipengele cha lazima cha ununuzi. (90min)

West Ham wamekubali ofa ya pauni milioni 15 kutoka kwa Fulham kwa ajili ya mlinzi wa Ufaransa Issa Diop, huku mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 akitarajiwa kusaini mkataba wa miaka mitano na The Cottagers. (Usajili unahitajika)

Issa Diop
Mlinzi wa Ufaransa Issa Diop

Fulham wamepewa ofa ya beki wa Ubelgiji Jason Denayer, 27, ambaye ni mchezaji huru baada ya mkataba wake na Lyon kumalizika. (Football insider)

Arsenal na Liverpool wameonyesha nia ya kutaka kumsajili winga wa Uhispania Yeremi Pino, 19, kutoka Villarreal. (AS – kwa Kihispania)

Kiungo wa kati wa Inter Milan na Croatia Marcelo Brozovic, 29, ndiye anayelengwa na Liverpool kama kiungo wa kati wa dharura. (Sport – kwa Kihispania)

Brozovic

Beki wa kushoto wa Uhispania Alex Moreno, 29, amekataa nafasi ya kujiunga na Nottingham Forest na atasalia Real Betis. (Guardian)

Monaco wana nia ya kumsajili beki wa Manchester United na Ivory Coast Eric Bailly, 28. (L’Equipe – kwa Kifaransa)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *