
Ralph Yarl mwenye umri wa miaka 16, alitumwa na wazazi wake kuwachukua kaka zake kutoka katika nyumba ya rafiki yao mnamo tarehe 13 Aprili, lakini akaenda kwa anwani isiyo sahihi.
Mshukiwa alimpiga risasi Bw Yarl akiwa katika mlango wake.
Kijana huyo alipiga risasi moja kichwani, imesema familia yake na mawakili wao.
Polisi imemwachia huru mtu aliyefyatua risasi kutoka kizuizini lakini hawajawatambua. Bw Yarl aliruhusiwa kutoka hospitalini Jumapili na anaendelea kupata nafuu akiwa nyumbani na familia yake, baba yake Paul Yarl aliliambia gazeti la Kansas City Star.
“Anaendelea kuimarika,” baba yake aliliambia gazeti. “
Mawakili mashuhuri wa haki za kiraia Ben Crump na Lee Merritt wanawakilisha familia ya Bw Yarl katika kesi hiyo. Waliwakosoa maafisa kwa kumwachilia huru mshukiwa, ambaye wanasema ni mwanaume mzungu.
“Huwezi tu kuwapiga watu risasi bila sababu kisa mtu anapokuja kugonga mlango wako – na kugonga mlango wako sio kosa. Huyu jamaa anapaswa kushtakiwa,” Bw Crump alisema.