image_2023-10-03_032401815

Klabu ya Ligi Kuu ya NBC ya Tabora United, zamani Kitayosce FC, yafungiwa kusajili kufuatia madai ya ada za usajili na malimbikizo ya mshahara kutoka kwa waliokuwa wachezaji wake, raia wa Ghana, Emmanuel Lamptey pamoja na Collins Gymfi.
Uamuzi huo uliofanywa na Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA), unakuja baada ya Wachezaji hao raia wa Ghana, kufungua na kushinda kesi dhidi ya waajiri wao wa zamani, klabu ya Tabora United.
Klabu hiyo ilikaidi amri ya kulipa madai ya wachezaji hao ndani ya siku 45 na kupelekea kufungiwa kusajili wachezaji kutoka nje ya mipaka na ndani ya Taifa la Tanzania.
Vilevile, klabu hiyo ilipewa adhabu sawa na hiyo wiki iliyopita baada ya kushindwa kumlipa aliyekuwa mchezaji wao, raia wa Ghana.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *