
Watumiaji wa Barabara ya Kasulu Kibondo Mkoani Kigoma, wameingiwa na Hofu baada ya Kukatika Miundombinu ya Barabara hiyo, Katika Kijiji na Kata ya Busunzu Wilayani Kibondo, ikiwa ni wiki kadhaa zimepita eneo hilo kuanza kupitika, hali ambayo imeacha maswali mengi kwa wananchi na watumiaji kwa kuhofia barabara hiyo kujengwa chini ya kiwango.