kigoma kmli sdasna

Mkoa wa Kigoma unatarajiwa kufanya Kongamano la Kibiashara litakalo jumuisha Nchi za Congo DRC, Burundi, Rwanda na Zambia lenye lengo la Kujadili na kuboresha hali za Kibiashara na uwekezaji mipakani baina ya Nchi hizo.

Akizungumza na waandishi wa habari Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Thobias Andengenye amesema watu miatano kutoka nchi hizo huku mia tatu kati yao wakileta bidhaa za maonyesho ambazo zinatarajiwa kuamsha hali ya biashara baina ya nchi hizo huku lengo ikiwa ni kuhakikisha changamoto zote zinazokabili biashara mipakani zinajadiliwa na kutatuliwa.

Kongamano la kwanza lilifanyika mwaka 2019 ambapo nchi za Congo DRC na Burundi zilihudhuria na tayari kuonyesha tija katika Biashara mipakani hivyo kuwa na umuhimu wa kuendelea kufanyika kwa maslahi mapana ya biashara baina ya nchi zote.

Kongamano hilo ambalo linatarajiwa kufanyika tarehe tisa mpaka kumi na moja mwenzi Mei mwaka huu Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Mh Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan.

#radiojoyupdate
#kigomafahariyetu
#somethingforeveryone

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *