
Polisi walitumia maji ya kuwasha na mabomu ya machozi kukabiliana na machafuko katikati ya jiji la Brussels siku ya Jumapili kufuatia ushindi wa 2-0 wa Morocco dhidi ya Ubelgiji katika Kombe la Dunia nchini Qatar.
Mashabiki kadhaa wa soka walivunja madirisha ya maduka, kurusha fataki na kuchoma magari.
Polisi walisema kuwa karibu watu 11 wamekamatwa.