Capture

Shirika la Joy In The Harvest na Radio Joy Fm, limetoa msaada wa magodoro 30 yenye thamani ya Shilingi milioni 1.5 kwa wafungwa wa Gereza la Bangwe lililopo Manispaa ya Kigoma Ujiji.

Akikabidhi msaada huo, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika hilo Mwenge Muyombi amesema wamefanya hivyo ikiwa ni baada ya Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Salum Kalli kutoa wito kwa mashirika yaliyopo Mkoani kusaidia kupunguza baadhi ya changamoto zilizopo kwenye gereza hilo hasa la ukosefu wa magodoro ya kulalia.

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Salum Kalli amepongeza shirika la Joy In The Harvest kwa kutoa msaada huo, huku akiongeza kuwa ushirikiano huo wa kuwahudumia wananchi ndio msingi wa maendeleo na kuomba mashirika mengine kuiga mfano huo.

Naye Mrakibu Mwandamizi wa Magereza, Mkuu wa Gereza la Bangwe Bakari Kasenga mbali na kutoa shukrani kwa msaada huo ameeleza baadhi ya mapungufu yaliopo kwenye Gereza hilo ikiwemo Magodoro na kuwa msaada huo waliopatiwa utasaidia kupunguza changamoto hiyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *