Capture

Bunge la Peru limemuondoa madarakani Rais Pedro Castillo na nafasi yake kuzibwa na makamu, Dina Boluarte muda mfupi baada ya Castillo kujaribu kulivunja bunge hilo, ikiwa kabla ya zoezi la kumpigia kura ya kumwondoa.
Ofisi maalumu yenye kuhusika na masuala ya uchunguzi nchini humo ilisema kitendo cha Castillo anaehusishwa na kupoteza udalifu kazini cha kujairibu kulivunja bunge ni sawa na tukio la mapinduzi.
Walipiga kura za ndio 101 na hapana 6 huku kura 10 kutokuwepo. Muda mfupi kabla ya kupigwa kwa kura hizo Castillo alitaka kuweka serikali ya dharura na kutaka duru ya pili ya mkutano wa bunge ya kufanikisha katiba mpya taifa hilo.

Katika hatua nyingine serikali ya Marekani ilisema imeupokea vyema uteuzi wa Bibi Boluarte kama Rais wa Peru, ambaye tayari ameapishwa na bunge la taifa hilo katika siku ambayo kulishuhudiwa kiongozi wa aliyeondolewa Castillo akitiwa nguvuni baada ya kufurushwa mamlakanai.

Taarifa ya wizara ya mambo ya nje imepongeza umadhubuti wa taasisi za Peru kwa kuhakikisha umadhubuti wa kidemokrasia na itaendelea kuliunga mkono taifa hilo chini ya serikali ya umoja wa kitaifa.
#somethingforeveryone

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *