
Polisi nchini Kenya wamewakamata walimu sita wa shule ya msingi katika eneo la magharibi mwa nchi kufuatia kanda ya video iliyoshirikishwa mitandaoni ikiwaonyesha wanafunzi wakiiga kitendo cha ngono huku wakiwatazama.
Taarifa za vyombo vya habari nchini humo zinaripoti kuwa walimu hao wa Nyamache, katika jimbo la Kisii, walikamatwa baada ya maafisa wa Wizara ya Elimu kutazama video hiyo na kutoa malalamiko.
Katika video hiyo, watu wazima wanaoshukiwa kuwa walimu wanasikika wakijadiliana na kucheka kwa sauti huku mtu akiwarekodi wavulana wanne ambao wamevalia sare za shule.
Video hiyo ilizua taharuki kwenye mitandao ya kijamii huku wengi wakitaka hatua zichukuliwe.(chanzo:BBC Swahili)