
Mlinda mlango wa Uturuki Ahmet Eyup Turkaslan amefariki dunia kufuatia tetemeko la ardhi lililotokea Jumatatu nchini kwao,
klabu yake ya Yeni Malatyaspor imethibitisha. Takriban watu 8,000 wamepoteza maisha nchini Uturuki na Syria kufuatia matetemeko ya ardhi.
“Kipa wetu, Ahmet Eyup Turkaslan, alipoteza maisha yake baada ya kukumbwa na tetemeko la ardhi. Pumzika kwa amani,”
klabu hiyo ilisema kwenye Twitter. “Hatutakusahau, mtu mzuri,” iliongeza. Turkaslan, 28, alichezea klabu ya daraja la pili ya Uturuki Yeni Malatyaspor mara sita baada ya kujiunga nayo 2021.