samia

Samia Suluhu Hassan,Rais wa Tanzania, amesema amepokea mapendekezo ya kikosi kazi cha kuratibu na kuchakata maoni ya wadau wa demokrasia, akisema Serikali inakwenda kuyafanyia kazi, “lakini mapendekezo yao si amri kwa Serikali.”

“Itabidi ndani ya Serikali tujipange vikosi kadhaa, wale watunga sheria, kuangalia mambo ya siasa na Katiba. Inabidi tujipange vikosi kadhaa ndani ya Serikali na pengine tuje tuwaombe tena baadhi yenu kuingia katika vikosi hivyo ili tuyafanyie kazi mlioyaleta.

“Kuna ambayo ni mepesi tunaweza kuyafanyia kazi haraka, lakini kuna yale ambayo lazima tukae na kuangalia sheria zilizopo zina mapungufu wapi? Na tunayabadilisha vipi kutokana na maoni yenu,” alisema Rais Samia.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *