HABARI POST

Kufuatia taarifa za kudaiwa kukamatwa kwa Askofu Mukombo Muyondi au Mulilege Mkombo Muyondi Kameka (Mzee wa Yesu) na maafisa wa Jeshi la uhamiaji limetoa taarifa kuwa mtu huyo amekuwa akiishi Nchini kinyume na sheria za Nchi.

Akizungumzia suala hilo, Msemaji wa Jeshi la Uhamiaji, SI-Paul Mselle amesema kuwa Askofu Mukombo Muyondi au Mulilege Mkombo Muyondi Kameka amefukuzwa Nchini ikidaiwa kuwa ni raia wa Congo ambaye anaishi Nchini kinyume na taratibu, ambapo imeelezwa kuwa jambo hilo limefanikishwa kwa ushirikiano kati ya Tanzania na Ubalozi wa Congo nchini

“Mara ya kwanza Mtuhumiwa aliondoshwa nchini mnamo Februari 02, 2011, mara ya pili Agosti 28, 2019 na sasa jana Mei 24, 2022 baada ya kubainika yupo tena Nchini mnamo Mei 15,2022” amesema Msemaji wa Jeshi la Uhamiaji, SI-Paul Mselle.

#somethingforeveryone
#kigomafahariyetu
#radiojoydigital

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *