watu

Takriban watu 46, wanaoaminika kuwa wahamiaji, wamepatikana wamefariki kwenye lori lililotelekezwa viungani mwa San Antonio, Texas.

Afisa wa zima moto alisema watu 16 wakiwemo watoto wanne pia wamepelekwa hospitalini.

Walionusurika walikuwa moto ‘’kugusika‘’ na wanakabiliwa na kiharusi cha joto na uchovu wa joto.

San Antonio, ambayo ni 250km (maili 150) kutoka mpaka wa Marekani na Mexico, ni njia kuu ya kupita kwa watu wanaosafirishwa kwa njia haramu.

Charles Hood, Mkuu wa Zimamoto wa San Antonio, alisema wahudumu wa dharura walifika katika eneo la tukio karibu 18:00 ndani (23:00 GMT) baada ya kupata taarifa za mtu aliyefariki.(BBC Swahili)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *