ks
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeendelea kusogeza huduma za afya karibu na Wananchi wa wilaya ya kasulu mkoani Kigoma kwa kuongeza idadi ya Zahanati, Vituo vya Afya na kuboresha hospital ya wilaya ya Kasulu Mlimani kuhakikisha jamii inapata huduma za afya kwa wakati nakuepuka kutembea umbali mrefu. Hayo yamebainishwa na Waziri wa nchi ofisi ya Waziri mkuu kazi, vijana, ajira na wenye ulemavu ambaye ni mbunge wa Jimbo la Kasulu mjini Mh, Profesa Joyce Ndalichako baada ya kutembelea kituo cha afya cha Kiganamo. Profesa Ndalichako amesema ujenzi wa Zahanati na Vituo vya afya ni mpango wa serikali kwa nchi nzima kuhakikisha wananchi wake wanapata huduma ya afya ya uhakika
Prof. Ndalichako
Kwa upande wake Mganga Mkuu wa halmashauri ya Mji Kasulu Dr Peter Janga amesema ujenzi wa zahanati na vituo vya afya na uboreshaji wa hospital ya wilaya ya kasulu imesaidia wananchi kupata huduma za uhakika na kutotegemea hospital ya wilaya pekee kama ilivyokuwa hapo awali.
Dr Peter Janga
Aidha Dr Janga amesema kwa sasa wananchi wa halmashauri ya Mji Kasulu wanapata huduma kwa wakati tofauti na ilivyokuwa awali ambapo wapo baadhi ya wagonjwa ili walizimu kusubiri kupata huduma mpaka siku mbili kufuatia changamoto iliyokuwepo mwanzoni.
Dr Peter Janga
Kwa upande wao baadhi ya wananchi kutoka halmashauri ya Mji Kasulu wamesema serikali imeendelea kutimiza ahadi yake kwa jamii kupata huduma za afya karibu
 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *