Waziri wa kilimo Hussein Bashe amewataka wananchi katika Kata ya Kagera manispaa ya Kigoma Ujiji mkoani Kigoma kutouza Ardhi yao ya kilimo katika Bonde la Mto Luiche ambalo limekuwa kitovu cha uchumi wao baada ya serikali kukabidhi eneo la mradi wa Umwagiliaji kwa mkandarasi ili kuanza ujenzi wa skimu ya kilimo cha umwagiiliaji
Waziri wa kilimo Hussein Bashe akiwa na mkurugenzi wa tume ya umwagiliajiRaymond Mndolwawakiwa katika mazungumzo mafupi wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa skimu ya Kilimo cha umwagiliaji.Picha na Tume ya umwagiliaji
Na, Emmanuel Michael
Sera ya Taifa siku zote imekuwa ni kukifanya kilimo kuwa sehemu ya mtanzania kujikwamua kiuchumi na ndio maana inaelezwa kuwa Kilimo ni Uti wa mgongo
Bonde la Mto Luiche limejumuisha wakulima mbalimbali wakiwemo wa mazao ya Mpunga , mahindi ,Mbogamboga na Mtunda nk.
Hili ni Bonde ambalo linatajwa kuwahudumia wakulima 9312 ambapo mradi huu wa umwagiliaji Luiche utajengwa na unajumuisha maeneo mawili ambayo ni skimu ya umwagiliaji na ujenzi wa bwawa la lita za ujazo laki 7 na kumi
Na hapa Wanufaika wa moja kwa moja ambao ni wakulima hapa wanaeleza namna ambavyo mradi huo unakwenda kuwanufaisha
Wakulima
Awali akisoma taarifa ya ujenzi wa mradio wa umwagiliaji Meneja Mradi wa Luiche Katuta Mustang amesema Mradi huo unatarajia kutumia shilingi Bilioni 60 na utatumia siku 720 sawa miaka mwili ili kukamilka ambapo ujenzi umeanza july 21 mwaka huu huku mkurugenzi mkuu wa Tume ya Umwagiliaji Raymond Mndolwa akisistiza juu ya utunzwaji wa mazingira
Mkurugenzi wa Tume
Aidha Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Thobias Andengenye amesema hatua hiyo kubwa kwa wakulima inakwenda kuongeza chachu ya maendeleo kupitia kilimo
Kwa upande wake Waziri wa Kilimo Hussein Bashe akawataka wananchi kutouza maneo yao kwa kurubuniwa kwani maeneo hayo thamani yake itawainua wao kiuchumi
Waziri wa kilimo Hussein Bashe
Eneo hilo Hekta 2800 zilimwa Mpunga,Mahindi Hekta 150 huku Bustani ya mbogamboga na Matunda ikiwa ni Hekta