Utekelezaji wa mradi wa uhifadhi wa mazingira katika vijiji vinne vinavyozunguka Hifadhi ya Msitu wa Makere Kusini na pori la Akiba la Moyowosi, katika Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma, unaotekelezwa na Shirika la TAWEA, umetajwa kuleta mabadiliko chanya katika shughuli za uhifadhi na utunzaji wa mazingira katika vijiji hivyo. Mradi huo umeendelea kuhamasisha wananchi kushiriki…