Biashara ni nguzo muhimu ya maendeleo ya wananchi na uchumi wa taifa. Katika Halmashauri ya Wilaya ya Uvinza, Mkoa wa Kigoma, wanawake wengi hujishughulisha na biashara ya chumvi kama njia ya kujipatia kipato na kukidhi mahitaji ya familia zao. Hata hivyo, changamoto ya ukosefu wa masoko ya uhakika imeendelea kuathiri biashara hiyo, jambo linalopunguza mapato yao na kudhoofisha ustawi wa familia…