rs

Rais SamiaSuluhu Hassan ameahidi kukamilisha miradi yote iliyoanzishwa na mtangulizi wake hayati rais John Pombe Magufuli .

Katika hotuba yake ya kumbukizi ya mwaka mmoja tangu kifo cha rais huyo wa awamu ya tano rais Samia alieleza yote ambayo mtangulizi wake aliyaenzi kama vile kuhakikisha nchi inajitegema na kupigana na rushwa.

‘’Nitaendeleza mema yote aliyotuachia Magufuli na kuleta mema mapya’’ rais Samia amesema.

Aliitaja baadhi ya miradi iliyokamilika ambayo ilianzishwa na hayati Magufuli ikiwemo

Daraja la Tanzanite jijini Dar-es-salaam na jitihada za kuboresha na kuendeleza huduma za maji ikiwemo afya,elimu na umeme

Rais Samia pia aliwahakikishia wenyeji wa Chato kwamba miradi yote huko chato itakamilishwa

‘’Ujenzi wa kivuko cha Chato umeshakamilika kwa asilimia 100 na ujenzi wa kiwanja cha ndege cha chato kipo kwa asilimia 95.

Miradi hii itakapokamilika nitakuja kuifungua mwenyewe kama angevyofanya rais Magufuli’ rais Samia alisema.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *