
mwanzo wa hotuba yake kurudia nadharia ambazo amekuwa akitumia mwaka mzima uliopita: anadai kuwa ni Washington ambayo “ilianzisha vita” na mapema mwaka 2022 iliitaka Ukraine kushambulia Crimea na Sevastopol.
Urusi, kulingana na Putin, “ilitumia na inaendelea kutumia nguvu kukomesha vita,” ambayo inadaiwa kuanzishwa nchi za Magharibi.
Putin alisema kuwa mnamo 1939 ” Nchi za Magharibi zilitoa nafasi” kwa wanajeshi wa Ujerumani ya Wanazi, na sasa inaendeleza “upinzani dhidi ya Urusi.”
Putin pia alisema kwamba alama za kijeshi za Wanazi zinadaiwa kutumiwa kwa wingi nchini Ukraine, na nchi za Magharibi “hazijali ni nani anashiriki katika vita dhidi ya Urusi”
”Hakuna mtu katika nchi za Magharibi anayezingatia majeruhi ya binadamu, kwa sababu matrilioni ya dola yamo hatarini,” Putin alisema.
Kuhusu masuala ya uchumi Putin anasema anataka kujenga mfumo salama wa malipo ya kimataifa ambao utapunguza utegemezi kwa nchi za Magharibi.
“Hatupaswi kurudia makosa yetu. Tusiharibu uchumi wetu”.