
Mahakama Kuu Dar es Salaam imetupilia mbali maombi ya Halima Mdee na wenzake kutokana na kuwepo kwa kasoro kuhusu jina la mjibu maombi wa kwanza.
Wajibu maombi walikuwa Bodi ya Wadhamini wa Chadema, Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG).
Chadema kupitia jopo la mawakili wake linaloongozwa na Peter Kibatala waliweka pingamizi wakiiomba Mahakama hiyo isiyasikilize maombi hayo, wakidai kuwa yana kasoro za kisheria huku wakibainisha hoja sita.
Mzozo wa nafasi za kibunge kwa wabunge hao zilianza mara tu baada ya uchaguzi wa mkuu wa mwaka 2020, ambapo Chadema ilipinga matokeao na ‘kususa’ kupeleka majina ya wabunge wa viti maaalumu kwa kile ilichoeleza kutoridhishwa na mchakato mzima wa uchaguzi, uliompa ushindi hayati John Magufuli.