
Watu saba wamefariki Dunia na wengine nane kujeruhiwa katika ajali iliyohusisha Lori na Bajaji jana Jumapili Machi 27,2022 katika eneo la mtaa wa Kidulya nje kidogo ya mji wa Bariadi.
Akizungumza na Waandishi wa habari Kaimu kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mkoani Simiyu Faustine Mtitu amesema chanzo cha ajali hiyo ni mwendokasi wa dereva wa Lori uliosababisha kugonga bajaji.
“Baada ya lori hilo kuigonga bajaji iliyokuwa imebeba abiria sita na lori likiwa na watu takribani 12, bajaji iliwaka moto na lori kupinduka” amesema Mtitu.