Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kaskazini mkoani Kigoma ameanzisha mashindano ya mpira wa miguu yenye lengo la mashindano hayo ni kukuza vipaji na kudumisha mshikamano miongoni mwa jamii. Na Sadick Kibwana Ligi ya mbunge wa Jimbo la Kigoma Kaskazini, Mhe. Kiza Mayeye (Mayeye Cup), imeanza rasmi Jumanne hii, Septemba 1, 2026, katika uwanja wa tarafa ya Mwandiga ikihusisha jumla ya timu 32.