
Siku ya jana Mei 20/2023 limefanyika tukio la kihistoria nchini Tanzania ambapo Rais wa Tanzania Samia suluhu Hassani amezindua Ikulu mpya ya Chamwino Dodoma ikihusisha lango la kuingia katika Jengo la Ofisi ya Rais Ikulu.
–
Kupitia mitandao ya kijamii imeibuka Mijadala mbali mbali huku baadhi ya Watanzania wakidai kuwa hawaelewi maana ya Bendera 3 zinazo pepea kwenye kilele cha Ikulu.
–
Hapa tumekuwekea maelezo na maana ya bendera hizo ambazo Baadhi ya Watanzania wengi wameshindwa kufahamu Tafsiri yake.
–
(1) Bendera ya Taifa ya Tanzania: Inajulikana kwa muundo wake unaohusisha rangi ya kijani juu, njano, na Nyeusi katikati chini Rangi ya Bluu. kijani inawakilisha uoto wa asili na maliasili za nchi, rangi ya njano inawakilisha utajiri na rasilimali za nchi, na Rangi Nyeusi inawakilisha Afrika chini kabisa ipo rangi ya Bluu ambayo inawakilisha Bahari na Visiwa. Hii ndio Bendera ya Taifa la Tanzania 🇹🇿
–
(2) Bendera ya Rais: Bendera hii inatumiwa Kwenye Shughuli za Rais. Ina muundo sawa na bendera ya taifa, lakini ina nyota ya kuashiria madaraka ya urais iliyowekwa upande wa kushoto wa juu ya bendera. Bendera hii inawakilisha uwakilishi wa Rais na mamlaka yake ndani ya Ikulu na nchi kwa ujumla.
–
(3) Bendera ya EAC Maana yake ni ‘Jumuiya ya Afrika Mashariki’ (East African Community) inatumiwa kuwakilisha umoja wa nchi wanachama wa Jumuiya hiyo, ambazo ni Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, na Sudan Kusini.
–
Bendera ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ina muundo unaofanana na bendera ya taifa ya Tanzania, lakini ina alama ya nembo ya Jumuiya ya Afrika Mashariki iliyowekwa katikati ya sehemu ya njano. Nembo hiyo inajumuisha ramani ya Afrika Mashariki, nyota saba zinazoashiria nchi wanachama, na shada la maua lenye rangi mbalimbali. Umoja huu pia unakuza mtiririko wa bidhaa, huduma, na mitaji kati ya nchi hizo wanachama, hivyo kuchochea ukuaji wa kiuchumi.