Zikiwa zimebaikia siku 12 kuelekea kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa mkuu wa wilaya ya kasulu kanal Isack mwakisu amewataka madiwani wilayani humo kuhakikisha wanakuwa mstari wa mbele kuwahimiza wananchi wajitokeze kuwachagua viongozi wao.
Mkuu wa wilaya ya kasulu kanal Isack Mwakisu akihutubia mkutano wa baraza la madiwani .Picha na Hagai Ruyagila
Kanal mwakisu amesema hayo katika mkutano wa baraza la madiwani kipindi cha robo ya kwanza ya july hadi septeber 24,25 ambapo amewaomba madiwani kuwashawishi wananchi bila kutumia nguvu ili kuhakikisha wanajitokeza kikamilifu siku ya uchaguzi wa serikali za mitaa.
Sauti yake Mkuu wa wilaya Kanal Isack Mwakisu
Aidha kanal mwakisu amewataka madiwani kuhakikisha wanaihubiri amani wakati huu wa uchaguzi ili kuepuka munyukano unaoweza kuhatarisha amani ya Tanzania.
Sauti yake Mkuu wa wilaya Kanal Isack Mwakisu
Naye mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya kasulu Bw,Elia kagoma amewaomba wagombea kutumia lugha nzuri na zaidi kueleza sera zao kuliko kutumia kauli zinazoweza kupelekea vurugu.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya kasulu BW. Elia Kagoma
Hata hivyo madiwani kwa ujumla wameaswa kuhakikisha wanazingatia r 4 za rais daktari samia suruhu hasani kwa kuhubiri ustahimilivu,usuruhishi, mabadiliko na kujenga upya umoja wetu.
watatu hupo chini ambao wamevaa sare za madiwani wa kati kati ni mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya bW, Elia Kagoma , wa mwisho kulia ni mkurugenzi wa halmashauri Bw, semistatus Mashimba