Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mheshimiwa Daktari Doto Biteko, ameagiza Wakandarasi wa uje nzi wa miradi ya kimkakati ya umeme mkoani Kigoma, kuongeza kasi ya utekelezaji ili miradi hiyo ikamilike kwa wakati na kusaidia katika kukuza uchumi wa watanzania na taifa.
Muonekano wa jengo la mitambo.Picha na Hamis Nterekwa
Akihutubia mamia ya wakazi wa mkoa wa Kigoma mara baada ya kuweka mawe ya msingi katika miradi mitatu ya umeme Kigoma, Ikiwemo mradi wa uzalishaji umee katika mto Malagarasi, Njia kuu ya kusafirisha umeme wa Gridi ya Taifa kutoka Nykanazi na Kituo cha kupoza umeme Kidakhwe, Mheshimiwa Naibu Waziri mkuu Daktari Doto Biteko, amesema miradi hiyo isaidie katika uwekezaji wa viwanda na kukuza uchumi Kwa wananchi.
Naibu Waziri mkuu Daktari Doto Biteko
Akitoa taarifa ya miradi ya umeme wa gridi ya Taifa, Mkurugenzi mtendaji shirika la umeme Nchini Tanesco Gissima Nyamahanga amesema miradi hiyo kukamilika kwake itakuwa chachu ya kuuza umeme hadi nchi jirani, huku viongozi wengine akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Thobias Andengenye wakieleza tija katika uwekezaji wa viwanda.
Mkurugenzi mtendaji shirika la umeme Nchini Tanesco Gissima Nyamahanga
..