Capture

Wazazi na Walezi katika Kata ya Buhanda Mkoani Kigoma wametakiwa  kuwalea watoto katika maadili mema na kuwapatia haki zao za msingi ikiwemo Elimu.

Hayo yameelezwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Joy in the Harvest, Mwenge Muyombi wakati wa mahafali ya huduma ya mtoto compassion kituo cha EAGT Mwasenga  kata ya Buhanda mkoani Kigoma ambapo amesema wazazi wanapaswa kutambua haki ya Elimu kwa mtoto.

Mh. Mwenge ameongeza kuwa wazazi na walezi wanatakiwa kuondoa dhana potofu na badala yake wawe na ushirikiano na vituo vinavyotoa Elimu na malezi kwa watoto ili kusaidia kuwapa malezi yatakayosaidia kuwakinga na mazingira hatarishi.

Kwa upande wake, Mratibu wa Elimu Kata ya Buhanda Mwl. Donatida Anacleti ameeleza kuwa wazazi wanapaswa kuhimiza watoto kufika shuleni ili kudhibiti wimbi kubwa la utoro kwa watoto.

Nao baadhi ya watoto walioshirki katika hafla hiyo wametoa rai kwa wazazi kuhakikisha wanafatilia mahudhurio na maendeleo yao ya Elimu  shuleni na kwenye vituo vya huduma ya malezi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *