
CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES
Real Madrid bado wana nia ya kumsajili mshambuliaji wa Ufaransa Kylian Mbappe kutoka Paris St-Germain lakini hawatalipa ada ya uhamisho wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24. (Marca In Hispanic)
Manchester United wanamwinda tena kiungo Adrien Rabiot huku Mfaransa huyo mwenye umri wa miaka 28 akikaribia mwisho wa mkataba wake na Juventus. (L’Equipe – In France )
Mauricio Pochettino anakaribia kusaini mkataba wa miaka mitatu kuwa kocha mkuu wa Chelsea. (Telegraph)

Meneja wa Brighton Roberto De Zerbi anatarajia kiungo wa Ecuador Moises Caicedo, 21, na kiungo wa kati wa Argentina Alexis Mac Allister, 24, kuondoka katika klabu hiyo msimu huu wa joto. (Metro)
Mshambulizi wa Uholanzi Wout Weghorst atafanya mazungumzo na meneja wa Burnley Vincent Kompany mara baada ya muda wake wa mkopo kumalizika Manchester United. (Sun)
Crystal Palace wana nia ya kumsajili mshambuliaji wa Lyon Mfaransa Moussa Dembele, 26, msimu huu wa joto. (Football Insider)
Manchester United wameungana na Arsenal katika mbio za kumsajili beki wa RB Leipzig Mfaransa Mohamed Simakan, 23. (Fichajes – In Spanish )
AC Milan bado wanataka kumbakisha kiungo wa kati wa Real Madrid raia wa Uhispania Brahim Diaz, 23, katika klabu hiyo msimu ujao. (Kalciomercato)
Mkewe Thiago Silva Belle amethibitisha kuwa beki huyo wa Brazil mwenye umri wa miaka 38 ananuia kusalia Chelsea msimu ujao. (Evening Standard)
Paris St-Germain wako tayari kufanya mkataba wao wa mkopo kwa mshambuliaji wa Ufaransa Hugo Ekitike, 20, kuwa wa kudumu lakini Eintracht Frankfurt bado wanavutiwa na mchezaji huyo. (L’Equipe – In France )