_114419397_d4430031-11fa-42f9-a27a-472ea91b53fd

Liverpool wamemfuatilia Ismaila Sarr na kujadili suala lake na Watford, ambayo inataka pauni milioni 36 kwa ajili ya mshambuliaji huyo.(Mail)

Sarr pia ametambulika na Manchester United kama mbadala ikiwa mpango wa kumnasa winga wa Borussia Dortmund Jadon Sancho utashindwa.(Independent)

Mashetani wekundu pia wanafikiria uhamisho wa winga wa Inter Milan Ivan Perisic, 31, Kingsley Coman,24 anayekipiga Bayern Munich na Douglas Costa kutoka Juventus. (ESPN)

Jadon Sancho alihamia Borussia Dortmund akitokea Manchester City mwaka 2017 kwa kitita cha pauni milioni 10

Manchester United wanamfuatilia kiungo wa kati wa Ujerumani Sami Khedira,33, mkataba wake na Juventus utakapokwisha. (Sun)

Wakala wa Edouard Mendy amedai kuwa makubaliano yameafikiwa kwa ajili ya mlinda mlango huyo, 28, anayekipiga katika klabu ya Rennes kujiunga na Chelsea. (Stades – via Star)

Brentford amekataa ofa ya takriban pauni milioni 10 kutoka Arsenal kwa ajili ya mlinda mlango David Raya, 25. (Telegraph)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *