Kuimarisha ulinzi na usalama husaidia kulinda maisha ya wananchi na mali zao na hali hii huwafanya wananchi kuishi na kufanya shughuli zao bila hofu. Na Orida Sayon Jeshi la Polisi Mkoa wa Kigoma limesema limejipanga kikamilifu kuhakikisha ulinzi na usalama wa raia pamoja na mali zao kwa kuendelea kudhibiti matukio ya uhalifu katika maeneo mbalimbali ya mkoa huo.