Capture
Rais wa Urusi Vladimir Putin anafanya mazungumzo na mkuu diplomasia wa Uchina Wang Yi.

Ziara ya Yi inakuja wakati Urusi ikiadhimisha mwaka mmoja wa vita pamoja na maadhimisho ya Siku ya Mlinzi wa Ardhi ya Baba inayofahamika kama – Defender of the Fatherland Day, ambayo inayoadhimishwa kesho.

Vyombo vya habari vya Urusi vilionyesha moja kwa moja sehemu ya kwanza ya mazungumzo ya kujitambulisha , ambapo rais wa Urusi alieleza jinsi mahusiano ya nchi mbili yanavyoendelea vyema, hususan katika sekta ya biashara.

Pia alimueleza kiongozi wa kamati ya masuala ya kigeni katika kamati kuu ya chama tawala cha Uchina, kwamba anategemea kufanya naye mazungumzo kuhusu hali ya kimataifa kwa sasa, ambayo aliielezea kuwa ngumu.

“Licha ya hali ya mzozo kimataifa, uhusiano wa Urusi na Uchina umeweza kuhimili shinikizo kutoka kwa jamii ya kimataifa na kuwa na maendeleo thabiti.Ingawa mzozo umekuwa ukiendelea, kuna fursa katika mizozo, na fursa pia hugeuka kuwa mzozo. Huu ni uzoefu wa kihistoria, na tunahitaji kutambua juhudi zetu katika kushughulikia mizozo na kuimarisha ushirikiano wetu ,” Wang Yi alijibu.

g

Mapema leo hii  mwanadiplomasia wa Uchina alikuwa tayari amefanya mazungumzo na Waziri wa mambo ya nje wa Urusi Sergei Lavrov.

“Hata hali za kimataifa zibadilike vipi, China imekuwa na itaendelea kujitolea, pamoja na Urusi, katika juhudi za kuimarisha maendeleo chanya ya uhusiano baina ya mataifa yenye nguvu zaidi,” Wang Yi talimwambia waziri wa Urusi, huku akimuelezea kama “rafiki yangu mpendwa.”

Kwa kutazama picha, Sergei Lavrov na katibu wa baraza la usalama Nikolai Patrushev pia wanashiriki katika mazungumzo ya Putin na mwanadiplomasia huyo wa Uchina.

Wachambuzi wamebaini kwamba Putin anakutana na mgeni wake katika ofisi ya Klemlin kwenye meza ndogo, badala ya meza kubwa ya mita -8 ambayo amekuwa akiitumia kwa kawaida kwa ajili ya mikutano na maafisa wa Urusi kwa kipindi cha miaka miwili iliyopita.

Kulingana na mwandishi wa BBC wa Uchina Stephen McDonell, kuonyesha kuwa wageni wanakutana naye kwa ukaribu lilikuwa ni jambo lililopangwa kwa makusudi ili kusisitiza kuwa kiongozi wa Urusi anahisi salama akiwa pamoja na mwakilishi wa rafiki muhimu wa Urusi.

Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali.

Katika mazungumzo baina ya viongozi hao wawili Putin amesema pia kwamba anasubiri ziara rais wa Uchina Xi Jinping.

haya yanajiri huku China ikifahamika kuwa mshirika muhimu zaidi wa kibiashara wa Urusi huku ikijaribu kupunguza athari za vikwazo vya kiuchumi ilivyowekwa na baadhi ya nchi ili kukabiliana na uvamizi wake nchini Ukraine.

Marekani iilisema pia kwamba makampuni ya China tayari yametoa “msaada usio wa kuua” kwa Urusi, na kwamba ina habari mpya zinazopendekeza Beijing inaweza kutoa “msaada hatari” hivi karibuni.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *