
Mkuu wa zamani wa The Blues, Lampard alikuwa kwenye viti kutazama sare ya bila kufungana na Liverpool, saa 48 tu baada ya Graham Potter kutimuliwa. Sasa mmiliki Todd Boehly anaweza kumgeukia Lampard kuchukua hatamu hadi mwisho wa msimu. Lampard, ambaye alikuwa mkufunzi wa Chelsea kwa miezi 17 na pia kuwa mfungaji bora wa klabu hiyo, amekuwa hana kazi tangu alipotemwa na Everton mwezi Januari. Msaidizi wa Potter Bruno Saltor alichukua jukumu la kuinoa The Blues Jumanne usiku lakini alikiri kuwa hajawahi hata kuchagua timu hapo awali.