
ARSENAL imeripotiwa kupata ofa ya pauni milioni 12 kwa siku ya mwisho ya kumnunua kiungo wa Chelsea Jorginho. Muitaliano huyo, 31, anatazamiwa kujiunga na The Gunners huku viongozi wa Ligi ya Premia wakihofia kuwasaka kwa muda mrefu nyota wa Brighton Moises Caicedo kunaweza kuishia kwa kutamauka.