Hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Kigoma Maweni imepokea mashine kwa ajili ya watoto njiti kutoka taasisi ya kupambana na kuzuia rushwa TAKUKURU Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) imekabidhi mashine mbili maalum kwa ajili ya kusaidia utoaji wa huduma kwa watoto waliozaliwa kabla ya muda, maarufu kama watoto njiti, katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kigoma Maweni.