Halmashauri ya Wilaya ya Uvinza imeendelea kuchukua hatua za kuongeza ushiriki wa makundi maalum katika zabuni na tenda za serikali kupitia mfumo wa manunuzi ya umma wa NeST, ikiwa ni sehemu ya jitihada za kuwawezesha wanawake, vijana, wazee na watu wenye ulemavu kunufaika na fursa za kiuchumi zinazotolewa na serikali. Mafunzo hayo yamefanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Uvinza…