wanawake

Mabingwa wa COSAFA kwa wanawake wenye umri chini ya miaka 17 wamerejea nyumbani na kufanyiwa hafla fupi ya kuwapongeza na kupewa zawadi ya Pesa.

Kamati ya Taifa Stars chini ya katibu wake Mhandisi Hersi Said ndio waliotoa zawadi hiyo zaidi ya Tsh 30 Milioni na kuahidi Makubwa.

”kamati yetu si kwa ajili ya Taifa Stars Pekee bali ni kwa ajili ya Timu zote za Taifa, kwa hiyo tumetoa kiasi hiki cha fedha kwa ajili ya mahitaji yenu madogo madogo lakini tunaahidi kufanya makubwa kwenu kadri mtakvyokuwa mkiendelea na mashindano tofauti tofauti.” Alisema

Timu hiyo ilitwaa ubingwa baada ya kuwafunga Zambia kwa mikwaju ya penati 4:3 baada ya Dakika 90 kumalizika wakiwa sare ya bao 1:1

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *