IMEELEZWA kuwa aliyekuwa Mtedaji Mkuu wa Klabu ya Simba, Senzo Mbatha anashikiliwa na Polisi katika kituo cha Oysterbay kwa tuhuma za kuihujumu Simba.
Habari zimeeleza kuwa anahojiwa kuhusu ishu ya kudaiwa kuihujumu timu yake ya zamani ili ipate matokeo mabovu kwenye mechi za ligi zilizopita.
Mbatha anadaiwa kufanya hivyo kwa kushirikiana na Hashim Mbaga, aliyekuwa mkurugenzi wa mashabiki na wanachama wa Simba ambaye naye alifutwa kazi.
Kwa sasa Mbatha ni mshauri mkuu ndani ya Klabu ya Yanga kwenye mchakato wa kuelekea mabadiliko ambapo aliibukia huko muda mfupi baada ya kubwaga manyanga ndani ya Simba.
Chini ya Kocha Mkuu Sven Vandenbroeck, Simba ilipokea vichapo kwenye mechi mbili mfululizo na kuyeyusha pointi sita ambapo ilikuwa dhidi ya Tanzania Prisons ilipopoteza kwa kufungwa bao 1-0 kisha ilipoteza kwa kufungwa bao 1-0 dhidi ya Ruvu Shooting.
Kutokana na matokeo hayo mabovu Simba ilifanya mabadiliko kwenye benchi la ufundi kwa kumuondoa Mohamed Mwarami aliyekuwa kocha wa makipa pamoja na Patrick Rweyemamu ambaye alikuwa ni Meneja wa Simba.
hata hivyo Senzo bado ni mtuhumiwa na ameachiwa na Jeshi hilo kwa Dhamana.