
SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limemtangaza Adel Amrouche kuwa Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa, Taifa Stars.
Amrouche ni raia wa Ubelgiji mwenye asili ya Algeria, ana uzoefu mkubwa wa soka la Afrika.
Amewahi kufundisha ukanda wa Afrika Mashariki ikiwa ni pamoja na Kenya pamoja na Ukanda wa Kusini Mashariki, Kati na Kaskazini.
Amewahi kuwa Kocha Bora wa Afrika Mashariki 2013 alipokuwa akiinoa Timu ya Taifa ya Harambee Stars na kuipa ubingwa wa CECAFA ambapo aliwahi kufika nusu fainali mara mbili akiwa na Burundi.
Kocha huyo amechukua mikoba ya Kim Poulsen raia wa Denmark aliyeachana na kikosi hicho Agosti mwaka jana ambapo kwa muda nafasi hiyo ilikuwa mikononi mwa Honour Janza.