Capture

Chama cha Mapinduzi (CCM) kimetangaza matokeo ya uchaguzi wa Washindi waliochaguliwa kuwa Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) kwenye viti 20 Tanzania Bara.

Kwa upande wa Wanaume Mshindi wa kwanza ni Mahenda Leonard aliyepata kura 845, nafasi ya pili ameishikilia Waziri Innocent Bashungwa mwenye kura 720 akifuatiwa na Steven Wasira mwenye kura 680 na Msome Jackson William kura 591.

Wengine ni Kasheku Msukuma (587), Kasesela Richard ( 574), Wambura Chacha Mwita kura 545, Waziri Bashe Hussein (510), Waziri Nape Nnauye (508), Askofu Josephat Gwajima (497), Waziri January Makamba (452), Waziri Mwigulu Nchemba (450), Macha (435) na Msengi Ibrahimu (428).

Upande wa Wanawake Dkt Angelin Mabula ana kura 770, Dkt Ashatu Kijaji (764), Christina Solomon Mndeme (761) , Hellen Makungu Kura 755, Fenela Mukangara ( 747) na Angellah J. Kairuki (730).

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *