
Waziri wa Maji Nchini Jumaa Aweso ameridhishwa na mradi wa chanzo Cha maji Amani beach mradi ambao unahudumia wananchi wa Manispaa ya Kigoma ujiji na maeneo ya mji mdogo wa mwandiga na Kazegunga.
Mh. Aweso amesema kukamilika Kwa mradi huo ni sehemu ya mkakati wa serikali kuhakikisha inawafikishia wananchi huduma ya maji na kuepukana na changamoto ya kutumia maji yasiyo salama.
Amesema lengo la Serikali ni kuhakikisha miradi yote ya maji ambayo ni ya kimkakati inakamilika na hatawavumilia watumishi waliopewa dhamana ya kusimamia miradi ya maji ambao hawatimizi wajibu wao.
Mh. Aweso yupo Mkoani Kigoma kwa ziara ya siku Tano ambapo mpaka sasa ametembelea miradi mbalimbali na kutoa maagizo Kwa wanaosimamia miradi kuwa waadilifu ili kuhakikisha inakamilika kwa wakati na kwa ubora unaotakiwa.